Usafi
Nafaka hukaguliwa na kusindikwa katika mazingira yanayolinda afya na ubora.
Kuhusu sisi
Nafaka Halisi ni kiwanda cha Arusha kinachounganisha wakulima wa ndani na familia, biashara na taasisi zinazohitaji bidhaa safi.
Hadithi yetu
Nafaka Halisi Tanzania ni kiwanda kilichosajiliwa nchini Tanzania kutoa huduma za usindikaji wa chakula katika mazingira yenye viwango vya juu vya usafi.
Tunashirikiana na wakulima wa kanda ya kaskazini kupata mahindi na ngano bora huku tukiwasaidia kupata soko la uhakika. Kupitia mitambo yetu ya kisasa, tunazalisha bidhaa zinazotumiwa na familia, mama lishe na viwanda vya mikate.

Misingi yetu
Nafaka hukaguliwa na kusindikwa katika mazingira yanayolinda afya na ubora.
Bidhaa zetu ni safi na hazichanganywi na vihifadhi vyenye madhara.
Tunawapa kipaumbele wakulima wazalendo na mahusiano ya muda mrefu.
Mizani sahihi, ufungashaji salama na mawasiliano ya wazi kwa wateja.
Viwango na ufungashaji
Tunanunua malighafi kutoka kwa wakulima wa ndani ili kuongeza thamani hapa nchini na kuleta chakula bora karibu na walaji.
Tazama bidhaa